30 Mei 2019 - 08:49
Marekani: Mashinikizo dhidi ya Iran yataendelea hadi Tehran ikubali mazungumzo

Msemaji wa Wizara ya Mashaurii ya Kigeni ya Marekani jana alisisitiza kuwa Washington itaendeleza siasa za kuishinikiza zaidi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

(ABNA24.com) Msemaji wa Wizara ya Mashaurii ya Kigeni ya Marekani jana alisisitiza kuwa Washington itaendeleza siasa za kuishinikiza zaidi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Morgan Ortagus amesema kuwa lengo kuu la serikali ya nchi hiyo kuzidisha mashinikizo kwa Iran ni kuishawishi Tehran iketi kwenye meza ya mazungumzo. Ortagus amesema kuwa Marekani inataka kufikia makubaliano mapya jumuishi na Iran. Marekani inatekeleza kampeni ya pande zote ya kuiweka chini ya mashinikizo Iran baad ya nchi hiyo kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Washington imesema kuwa inatekeleza kampeni hiyo ya kuiwekea Iran mashinikizo zaidi ili kufikia makubaliano mapya na Tehran ambayo ndani yake kutajadiliwa masuala yote yanayotakiwa na Marekani. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana alasiri  alikutana na kuzungumza na maelfu ya wahadhiri na wawakilishi wa kamati za kielimu za Vyuo Vikuu vya Iran na kulitaja suala la mazungumzo kuwa ni mbinu inayotumiwa na Marekani ili kukamilisha stratejia ya mashinikizo dhidi ya Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha alisisitiza kwa mara nyingine tena kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitafanya kabisa mazungumzo na Marekani na kueleza kuwa: Kama nilivyobainisha pia hapo awali sababu ni kuwa, kufanya mazungumzo na Marekani kwanza hakuna faida yoyote na pili, kuna madhara.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumanne tarehe 14 mwezi huu pia alikuwa na mazungumzo na viongozi na maafisa wa mfumo na kusisitiza kuwa chaguo la wazi la wananchi wa Iran ni kuendesha mapambano dhidi ya Marekani na katika makabiliano hayo Marekani itarudi nyuma. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi muhimu katika kukabiliana na njama na hatua za ushari za Marekani, Saudi Arabia na Wazayuni katika eneo. 




/129